Mkuu wa haki wa UN ashtushwa na mauaji ya kiholela Sudan
3 Aprili 2025Matangazo
Turk amesema afisi yake imekuwa ikitazama mikanda ya "kutisha" ya video katika mitandao ya kijamii tangu Machi 26 inayoonyesha watu waliojihami wakiwauwa raia kusini na mashariki mwa Khartoum.
Haya yanafanyika wakati ambapo wanamgambo wa RSF leo wamesema wameidungua ndege ya kijeshi Antonov inayomilikiwa na jeshi la Sudan.
RSF imesema imechapisha video iliyoonyesha mabaki ya ndege hiyo ingawa shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha picha hizo.
Maafisa wa jeshi la Sudan hawakupatikana wakati huo kutoa kauli kuhusiana na madai hayo ya shambulizi la RSF.