Rais William Ruto wa Kenya amemteua Erastus Ethekon kuwa Mwenyekiti ajaye wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC. Msomi huyu na mwanasheria anashika wadhifa huu katikati ya changamoto nyingi zinazoikabili tume hiyo ikiwa ni pamoja na kutoaminika kutokana na changamoto kwenye uchaguzi wa siku za nyuma. Lilian Mtono amezungumza na Barack Muluka, mchambuzi wa masuala wa siasa kuhusu uteuzi wake.