Mkutano wa wafadhili wa Syria wafanyika mjini Brussels
17 Machi 2025Matangazo
Ujerumani imeahidi kutoa nyongeza ya msaada wa yuro milioni 300 huku Uingereza ikiahidi kutoa dola milioni 200 ili kuisaidia Syria kupunguza athari za vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoikumba nchi hiyo kwa miaka kadhaa.
Fedha hizo zitasaidia kwenye utoaji wa misaada ya kibinadamu, elimu, mashirika ya kiraia na kuwasaidia wakimbizi wa Syria na jamii zinazowahifadhi katika mataifa ya Jordan, Lebanon, Iraq na Uturuki.
Soma pia:Marekani yasifu makubaliano kati ya serikali ya Syria na Wakurdi
Akizungumza kwenye mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amelaani vurugu za hivi karibuni katika jimbo la pwani la Latakia, na kuitaka serikali ya mpito ya Syria kufanya uchunguzi.