Mkutano wa usalama mjini Munich waingia siku yake ya mwisho
16 Februari 2025Masuala mengine muhimu yatakayozungumzwa ni kuyajumuisha haraka mataifa ya Balkan katika Umoja wa Ulaya na Ushindani wa Ulaya.
Tangu siku ya Ijumaa mkutano huo umekuw ukijadili hatua mpya za serikali ya Trump katika vita vya Ukraine na migongano juu ya ushiriki wa ulaya katika mazungumzo yoyote ya amani ya Ukraine.
MSC 2025: Mkutano wafunguliwa huku Marekani ikishinikiza kumaliza vita vya Ukraine
Siku ya kwanza ya mkutano huo naibu rais wa Marekani JD Vance aliwakosoa vikali washirika wake wa Ulaya akiwashutumu kwa kubinya Uhuru wa kujieleza aliyosema hali hiyo inaweka demokrasia hatarini.
Amekosoa pia hatua ya kukizuwia chama cha siasa kali nchini Ujerumani cha (AfD) na kile cha kipopulisti cha Muungano wa Sahra Wagenknecht kushiriki katika mkutano huo.