Mkutano wa jumuiya ya NATO,waanza The Hague
24 Juni 2025Matangazo
Viongozi wa ulimwengu wamekusanyika leo mjini The Hague nchini Uholanzi, katika mkutano wa kilele wa kihistoria wa siku mbili wa Jumuiya ya kujihami ya NATO.
Mkutano huo huenda ukayaunganisha au kuzidisha mgawanyiko miongoni mwa mataifa wanachama wa jumuiya hiyo kubwa ya kiulinzi duniani, kuhusiana na suala la kutoa ahadi mpya ya bajeti ya ulinzi.
Nchi washirika 32 wa mfungamano huo wa NATOwanatarajiwa kuidhinisha lengo la uchangiaji asilimia 5 ya pato jumla la ndani ya mataifa yao,kusimamia bajeti ya usalama.
Hatua hiyo inadhamiria kuziwezesha nchi hizo kutimiza mipango yao ya kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka nje.Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Mark Rutte amesisitiza kwamba mkutano huo utajadili pia vita vya Ukraine.