Juhudi za kupambana na uchafuzi wa plastiki zaendelea Geneva
5 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na takwimu za Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, tani zipatazo milioni 500 za plastiki zilizalishwa duniani kote mwaka 2024, takribani milioni 400 ambazo ziliishia kuwa taka.
UNEP imeonya kuwa bila makubaliano, kiasi cha taka kinaweza kuongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2060.
Mwezi Machi, mwaka 2022, Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa lilikubaliana kuujadili mkataba wa kupambana na uchafuzi wa plastiki.
Hata hivyo, miaka mitatu ya majadiliano iligonga mwamba Korea Kusini mwezi Desemba, 2024 wakati kundi la mataifa yanayosafirisha mafuta kwa wingi duniani lilipozuia makubaliano.
Inatarajiwa kuwa mkataba huo unaweza kusainiwa mwaka ujao.