Mkutano wa kujadili vita vya Ukraine wafanyika mjini Paris
17 Aprili 2025Mkutano huo utajadili pia kukwama kwa juhudi za amani zilizoanzishwa na rais wa Marekani Donald Trump.
Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, mjumbe maalumu wa Rais Donald Trump, Steve Witkoff, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na waziri wake wa mambo ya nje Jean-Noel Barrot, huku Ukraine ikiwakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje Andrii Sybiha na mkuu wa ofisi ya Rais Andriy Yermak.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatolea wito viongozi wanaoshiriki mkutano huo wa Paris kuzidisha shinikizo kwa Urusi ili kukomesha vita na kuhakikisha amani ya kudumu. Kwa upande wake, msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov ameupuuza mkutano huo akisema kwa bahati mbaya nchi za Magharibi zinajikita zaidi katika kuendeleza vita.