Mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi mjini Riyadh,Saudi Arabia
8 Februari 2005Mabingwa kutoka nchi mbali mbali walijadiliana juu ya aina mbali mbali za ugaidi na ujumbe wa Ujerumani ulikuwa na maafisa kutoka wizara ya mambo ya kigeni, wizara ya mambo ya ndani na idara ya upelelezi.
Mmoja kati ya watu walikuweko katika kufunguliwa mkutano huo hapo Februari 6 ni balozi wa Tanzania katika Saudi Arabia, Mohammed Mzale, na nilimpigia simu baadae kumuuliza kama neno lenyewe ugaidi ambalo limekuwa likileta mabishano juu ya tafsiri yake lilipata maana yenye kukubalika huko Riyadh:
Insert: 0 Ton...Mohammed Mzali...
Wenyeji wa mkutano huo, Wa-Saudi, walichukuwa jitihada ya kuelezea kwamba mizizi ya ugaidi haitokani huko Saudi Arabia na haiko katika Uislamu. Kwa hakika, Saudi Arabia imebeba mzigo mkubwa wa kushambuliwa na magaidi na imejiunga kuwa kati ya nchi za mstari wa mbele katika kupambana na ugaidi. Watayarishaji wa mkutano wa Riyadh walishikilia kwamba Osama Ben Laden na kumi na tano kati ya watu kumi na tisa walioshiriki katika mshambulio ya Septemba 11, mwaka 2001 huko Marekani walikuwa na asili ya Saudi Arabia ni jambo lisilokuwa na umuhimu. Walidai kwamba Osama Ben Laden hajawahi kuwa gaidi wakati alipokuwa anaishi Saudi Arabia. Kushiriki kwake katika vita vya kuikomboa Afghanistan kutoka kwa wavamizi wa Kirussi kulikubaliwa, kimataifa, na ni baadae pale yeye na wafuasi wake waliposhawishiwa na duru zenye siasa kali. Pia Saudi Arabia kwa zaidi ya miaka kumi sasa imemkana Osama Ben Laden na imemvuwa uraia wa nchi hiyo.
Kwamba chimbuko la ugaidi haliko Saudi Arabia na Uislamu sio alama ya ugaidi ni jambo linalokubalika. Lakini kwa kiasi gani Saudi Arabia imeathirika na ugaidi wenyewe? Balozi wa Tanzania katika ufalme huo, Mohammed Mzale, aliniambia hivi:
Insert: O Ton...Mohammed Mzale....
Huko Saudi Arabia Sheikh Saleh Abdel azizi al-Sheikh ni waziri wa masuala ya dini na yeye anasisitiza kwamba ugaidi hauambatani kwa vyovyote na Uislamu. Yule ambaye anawauwa na kuwajeruhi watu wasiokuwa na hatia, yule ambaye anaharibu mali za watu, basi anakwenda kinyume na moja wapo ya misingi muhimu ya Uislamu. Saudi Arabia inajitahidi kupambana na watu hao walio na siasa kali kwa njia mbali mbali. Katika nchi hiyo kumetolewa miongozo ilio wazi kwamba Maimamu wa misikiti wahubirie amani, ustahamilivu na mdahala. Imamu ambaye hafuati maagizo hayo, basi hubadilishwa.
Waziri huyo anasema kuwa na mdahala na watu wenye siasa kali ni mkakati mwengine:
Insert: O Ton...
+Wizara imefungua mdahala kwa njia ya mtandao wa Internet, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 800 wameshiriki, na zaidi ya robo moja kati yao wameshazikubali hoja za serekali.+
Wanaoshiriki katika mdahala huo hawajitaji na mtu hawezi kujuwa wanaandika kutokea wapi. Masuali na maoni yao hufanyiwa kazi na mabingwa katika wizara ya mambo ya dini; hivyo kunapatikana mdahala wa kusisimua na wenye tija. Pia inatarajiwa kwamba watu zaidi watasogezwa katika njia ilio sawa. Si tu kuna mdahalo wa aina hiyo na watu wasiojitambulisha wenyewe, lakini pia kunaendeshwa mazungumzo na watu wanaoshukiwa kuwa ni magaidi na wale walioko magerezani kwa makosa ya ugaidi ili kuwakomboa na kuwashawishi wajivuwe na fikra na nadharia zao potofu.
Waziri al-Sheikh anasema kazi hiyo sio rahisi, kwani kila pahala duniani kuna watu wenye siasa kali na wale wenye siasa za wastani. Yeye anasema kwamba serekali ya Saudi Arabia imeamuwa kuwaunga mkono na kuwasaidia wale wanaofuata siasa za wastani na kuwapinga kwa nguvu zote wale wenye siasa kali.
Pia haikataliki kwamba kuna sababu mbali mbali za kuchomoza ugaidi katika eneo lolote. Mohammed Mzale, balozi wa Tanzania katika Saudi Arabia, alinifahamisha kama hivi:
Insert: 0 Ton.... Mohammed Mzale...
Mkutano wa Riyadh umeacha kujishughulisha na kutafuta tafsiri ya neno ugaidi na kuuwachia mzigo huo Umoja wa Mataifa. Lakini kuna wahakiki wanaosema kwamba bila ya kukubaliana na maana ya neno ugaidi, hatutaepukana na mabishano wakati wa kutathmini kisa chochote kinachonukia harufu ya ugaidi.
Kama mkutano wa Riyadh utasaidia chochote katika mikakati ya siku za mbele ya kupambana na aina za ugaidi, balozi Mohammed Mzale alisema hivi:
Insert: O-Ton ...Mohammed Mzale....
Miraji Othman