Mkutano wa kimataifa juu ya plastiki wafanyika Geneva
5 Agosti 2025Matangazo
Mwakilishi wa Sychelles inayoongoza mataifa mengine 39 ya visiwa, Angelique Pouponneau, alisema mkutano huo unaoanza leo mjini Geneva ndiyo fursa ya mwisho ya kutenda kitu sahihi kwa sayari ya dunia.
Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Inger Andersen, alisema bado kuna masuala kadhaa yanayokwamisha kufikiwa kwa makubaliano hayo, ingawa amekiri kwambamgogoro wa kimazingira unaosababishwa na plastiki ni mkubwa na wa hatari kwa ulimwengu.
Baina ya tani milioni 19 na 23 za takataka za plastiki huingia kwenye mifumo ya maji ulimwenguni kila mwaka, na endapo hatua hazikuchukuliwa, Umoja wa Mataifa unasema uchafu wa plastiki utafikia asilimia 50 ya uchafu wote baharini ifikapo mwaka 2040.