Mkutano wa Bayoanuai waingia siku ya mwisho
27 Februari 2025Matangazo
Rais wa mkutano huo unafanyika mjini Roma, Italia, Susana Muhamad amewarai wajumbe wanaohudhuria kufanya kazi pamoja ili kupata makubaliano yanayowezesha kuilinda mifumo ya ikolojia na viumbehai inayotegemewa kwa maisha ya binadamu.
Mkutano huo uliofunguliwa Jumanne wiki hii umefanyika karibu miezi minne tangu wajumbe waliposhindwa kuafikiana kuhusu mgawanyo wa fedha miongoni mwa mataifa masikini walipokutana Novemba mwaka jana mjini Cali, nchini Colombia.
Mazungumzo ya Colombia yalidhamiria kuanzisha utakelezaji wa Mkataba wa Kimataifa kuhusu ulinzi wa Bayoanuai uliotiwa saini mwaka 2022. Mkataba huo umeweka malengo 23 yanayopaswa kutimikizwa ifikapo mwaka 2030 ikiwemo kuhifadhi angalau asilimia 30 ya maeneo yote ya nchi kavu na bahari.