Mkutano wa akili mnemba wafanyika Paris
10 Februari 2025Wakuu wa nchi, viongozi wakuu wa serikali, wakurugenzi wakuu na wanasayansi kutoka karibu nchi 100, wanashiriki katika mkutano huo wa kimataifa utakaoanza leo Jumatatu.
Wageni mashuhuri wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na makamu wa Rais wa Marekani JD Vance, hii ikiwa ni hafla yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuingia madarakani, pamoja na waziri mkuu wa China Zhang Guoqing.
Wakati huo huo, katika hotuba aliyotoa jana kupitia televisheni ya taifa France 2, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, alisema dunia inaishi katika mabadiliko ya kiteknolijia na kisayansi yasioshuhudiwa mara kwa mara.
Rais huyo ameongeza kuwa Ufaransa na Ulaya lazima zitumie fursa hiyo kwasababu teknolojia ya akili mnemba itawawezesha kuishi vyema, kujifunza vizuri zaidi, kufanya kazi vizuri, kujali vizuri na kuongeza kuwa ni jukumu lao kutumia teknolojia hiyo kwa huduma kwa binadamu.