Mkutano mgumu wa kilele wa Jumuiya ya Ulaya mjini Brussels hii leo
16 Juni 2005
Baada ya wapiga kura wa Kifaransa na Kiholanzi kuikataa katiba ya Ulaya, Jumuiya ya Ulaya sasa iko katika mzozo mkubwa. Haitarajiwi kwamba kutapatikana muelekeo wa mambo yatakavokuwa, licha ya kuanza leo mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya hiyo. Hali ya kutojuwa la kufanya ni kubwa mno tangu mkataba wa katiba ya Ulaya kukataliwa na nchi mbili hizo. Hali kama hii haijawahi kutokea. Pia kuna tafauti kubwa baina ya nchi wanachama kuhusu bajeti ya Jumuiya. Zaidi anayo...