SiasaSudan
Mkutano kati ya nchi nne kuhusu Sudan waahirishwa
30 Julai 2025Matangazo
UAE na Misri zinazochukuliwa kama washiriki wakuu wa kigeni katika mzozo wa Sudan, zimetofautiana kuhusu nafasi ya jeshi na wanamgambo wa RSF katika kipindi cha mpito wa kisiasa.
UAE inataka pande zote mbili ziondolewe kwenye mchakato huo, lakini Misri ikasisitiza kulindwa kwa taasisi za taifa hilo ikiwemo jeshi.
Hayo yanajiri wakati ambapo muungano unaoongozwa na kundi la RSF ulitangaza siku ya Jumamosi serikali pinzani huko Sudan , hatua iliyopingwa vikali na Umoja wa Afrika uliozitaka nchi zote wanachama na jumuiya ya kimataifa kutoiunga mkono ukisema unahatarisha mchakato mzima wa amani na mustakabali wa Sudan.