MKENYA PAUL TERGAT AWEKA REKODI MPYA YA DUNIA YA MBIO ZA MARATHON BERLIN
29 Septemba 2003Matangazo
- STUTTGART IMEPARAMIA TENA KILELENI MWA BUNDESLIGA-LIGI YA UJERUMANI
- NA MICHAEL SCHUMACHER YUKO POINTI 1 TU KABLA KUVAA TAJI LAKE LA 6 LA DUNIA LA MBIO ZA MAGARI.
Tergat aliifuta rekodi hiyo kwa muda wa sek.43.Tergat ambae mara nyingi humaliza nafasi ya pili katika mashindano makuu ya dunia,aliwajibu wale waliosema-jawezi kushinda mbio kuu-kwa kusema alijuan siku yake itafika ya kunyakua ushindi.na kweli jana ilifika mjini berlin akiwa na umri wa miaka 34.Kwani,Tergat mara mbili aliibuka makamo-bingwa wa Olimpik katika mita 10.000 akishindwa na Muethiopia Gebereselassie tangu katika michezo ya Atlanta ya Olimpik,1996 hata ile ya Sydney,Australia,2000 iliojionea changamoto kali kati ya wababe hao 2 wa medani ya riadha.
Paul Tergat alimaliza wapili pia katika mbio za London Marathon mwaka 2002 akishindwa na Khannouchi.Pia alitokea wapili katika mbio za marathon za London na chicago 2001.Licha ya ushindi wake mkubwa katika medani ya riadha unaojumuisha ubingwa mara 5 wa mbio za nyika duniani-world-cross-country championships,Paul terget akikosolewa nyumbani Kenya kwa daima kuwa katika kivuli cha Gebereselassie na Khalid Khannouchi.Kuanzia jana mjini berlin, hayo yamekwisha na jinsi alivyofurahia ushindi wake-paul Tergat aliambia Radio DW mwishoni mwa mbio hizo za kusisimua za marathon hivi:
Paul Tergat akijibu wapi rekodi ya dunia ya mbio za marathon siku za mbele itasimama:alisema siku moja rekodi hiyo alioipunguza kwa sek.43 jana, inaweza ikawekwa katika muda wa masaa 2:04:40 au hata masaa 2:04:30 lakini haamini kwamba,itaweza kushushwa chini ya masaa 2:04:20.
Jogoo mwengine alietikisa dunia jana,alikua mjerumani Michael Schumacher akiendesha gari la FERRARI katika mashindano ya Grand Prix ya marekani huko Indianapolis.Schumacher aliwapiku maadui zake na kumaliza wa kwanza na sasa yuko pointi 1 tu kabla kutwaa taji lake la 6 la ubingwa wa dunia-hii ikiwa rekodi.Nafasi ya pili jana alikuja Mfinland Kimi Raikkonen akiendesha gari la McLaren huku Heinz-Herald Frentzen akija 3.Michael Schumacher sasa ana jumla ya pointi 92 wakati Raikkonen pointi 83.Mcolumbia alietazamiwa kutoa changa moto kali kwa Schumacher Juan pablo Montoya alieanza mbio za jana akiwa nafasi ya pili nyuma ya Schumacher,alijionea matumaini yake ya ushindi yakitoweka alipomaliza 6 katika gari la Williams.
BUNDESLIGA:
LIGI YA UJERUMANI ilimalizika jana jioni huku VFB Stuttgart akiparamia kileleni tena mwa Ligi hiyo baada ya kuizaba Munich 1860 mabao 3:0.Mkiani mwa Ligi inajikuta FC Cologne iliochezeshwa jumamosi nyumbani kindumbwe-ndumbwe na Werder Bremen na kuchapwa mabao 4:1.Sasa hatima ya kocha wao imo mashakani,endapo Cologne ikishindwa tena jumamosi ijayo na viongozi wa Ligi-Stuttgart,basi kuna uwezekano mkubwa akatimuliwa.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ,waliitimua Rostock kwa mabao 2:1 na wameasngukia nafasi ya 4 katika ngazi ya Ligi.Kufuatia ushindi wao dhidi ya FC Cologne, Bremen iko nafasi ya pili huku Bayer Leverkusen ilioishinda Wolfsburg kwa bao 1:0 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya viongozi Stuttgart.Jana Hertha Berlin ilimudu suluhu tu bao 1:1 na Hamburg wakati Schalke iligawana pia pointi na Frankfurt kwa kuondoka uwanjani sare bao 1:1.
Matangazo