Gavana wa kaunti ya Nakuru amezindua mradi wa mkaa utokanao na kinyesi cha binadamu, maarufu kama makaa dot com. Mkaa huo unaotumiwa kupikia majumbani na kwenye shughuli za viwanda umetajwa kuwa uvumbuzi wa kipekee.
Nia ya mradi huu ni kuhifadhi mazingira, kupunguza gharama ya matumizi ya mkaa na kuimarisha hali ya afya pamoja na usafi. Ni mradi ambao wadau wa kaunti ya Nakuru wanapanga kuupigia debe kote nchini kwa manufaa ya wengi. Mwandishi wetu kutoka Nakuru Wakio Mbogho ana taarifa zaidi.