Mjumbe wa UN alaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Syria
3 Mei 2025Matangazo
Hayo yanajiri wakati Israel ikisema wanajesi wake iliyowapeleka Kusini mwa Syria wako tayari kuilinda jamii ya walio wachache ya madhehebu ya Druze katika kuzuia vikosi vya adui kuingia kwenye vijiji vyao.
Soma zaidi: Israel yafanya mashambulizi mjini Damascus
Israel imekuwa ikifanya mashambulizi ya kisasi Syria baada ya shambulio la Jumatano lililosababisha vifo vya watu 35 wa jamii hiyo. Vikosi vya usalama vya Syria na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wanatajwa kuwa walifanya shambulio hilo.
Watu wa jamii ya Druze wanaishi kwenye nchi za Syria, Lebanon, Israel na Jordan. Jamii hiyo inaheshimika Israel na sehemu ya watu wake wanalitumikia jeshi la nchi hiyo.