MigogoroMashariki ya Kati
Mjumbe wa Trump kwa Mashariki ya Kati awasili Israel
31 Julai 2025Matangazo
Witkoff atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kujadili tatizo la uhaba mkubwa wa chakula ambalo limeendelea kuzusha ukosoaji mkubwa kimataifa.
Aidha, Waziri wa mambo ya Nje Ujerumani Johann Wadephul ameelekea pia Israel kwa mazungumzo na Netanyahu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar. Wadephul ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza na kuitaka Israel kuboresha hali ya kibinadamu.
Hayo yanaripotiwa wakati shirika la ulinzi wa kiraia la Gaza limesema makumi ya Wapalestina wameuawa wakati vikosi vya Israel vilipofyatua risasi kwa umati wa watu waliokuwa wakigombea misaada.