Mjumbe wa Marekani aitaka Rwanda kuondoa wanajeshi wake DRC
17 Aprili 2025Aidha mjumbe huyo ameitaka Kigali kusitisha aina yoyote ya msaada kwa kundi la waasi la M23. Massad Boulos ameitoa kauli hiyo baada ya kukutana wiki hii na viongozi wa nchi zote mbili.
Hayo yanajiri wakati mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika nchi za maziwa makuu Xia Huang amesema eneo hilo bado limenaswa katika mzozo uliokithiri na unaochochewa na uhasama wa kisiasa, makundi ya wapiganaji na uchu wa rasilimali, akisisitiza kuwa ni lazima kuweko na juhudi zaidi ili kurejesha hali ya utulivu nchini Kongo.
Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Kongo, Therèse Kayikwamba aliuambia jana mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota mashariki mwa Kongo, huku akitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka.