Mjumbe maalum wa Marekani akutana na viongozi wa Ukraine
20 Februari 2025Matangazo
Ziara ya mjini Kiev, ya mjumbe huyo wa Marekani, imefanyika katika kipindi kigumu linapohusika suala la diplomasia kwa Ukraine, baada ya Rais Donald Trump, kuanza mazungumzo na Urusi na kumuondowa Rais Vladmir Putin kwenye nafasi ya kutengwa kisiasa na jumuiya ya Kimataifa.
Soma pia:Rais Donald Trump amuita Zelensky Dikteta
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine , amesema usalama wa nchi yake sio suala la mjadala.
Mjumbe Marekani, Keith Kellog ambaye pia ameshakutana na kamanda wa ngazi za juu wa Ukraine na viongozi wa ujasusi na idara za usalama wa nchi hiyo, atakutana pia na Rais Volodymyr Zelensky.