MJADALA WAPAMBAMOTO JUU YA SURA YA UBEPARI UJERUMANI
4 Mei 2005Gazeti la Offenburger Tageblatt laandika:
„Mjadala juu ya swali muhimu kabisa kuhusu hatima ya nchi hii kwa matamshi aliotoa mwanahistoria Michael Wolffsohn, umefikia daraja ya soga la m kahawani.Mtaalamu huyu amelinganisha ila juu ya ubepari zilizotolewa na mwenyekiti wa chama-tawala cha SPD Franz Münterfering, kuwa sawa na uchochezi dhidi ya wayahudi za enzi ya utawala wa Manazi.Katika jukwaa lolote la mazungumzo,Bw.Wolffsohn angepig iwa makofi kwa matamshi yake hayo.Lakini katika medani ya vita vya kupambana na ukosefu wa nafasi za kazi,asiachiwe uwanja –lausia gazeti la OFFENBURGER TAGEBLATT.
Gazeti la Hamburg:MORGENPOST linaandika kwamba, hadi sasa mjadala huu juu ya sura ya ubepari nchini Ujerumani ukidorora mpaka pale ulipochangamishwa hadharani na Bw.Müntefering,alipoulinganisha ubepari na panzi wanaotishia kuteketeza mimea.Alao hadi jana, mjadala huu umeanza sasa kutovumilika.Mwanahistoria ambae kamwe hakuwahi kugonga vichwa vya habari juu ya mada za kihistoria,kwa matamshi ya kipumbavu na ya uchochezi ,ameunyanganya mjadala mzima maana yake-laandika gazeti hilo la Hamburg.
Ama gazeti linalotoka mjini Kassel la Hessische-Niedersächsische ALLGEMEINE linauona mjadala huu kuhusu ila juu ya ubepari alizotoa Bw.Franz Münterfering yamkini mtu akaiangalia kwa jicho la juu juu tu bila kiini, au wa kutaka kujikomboa na hata kuchangamsha siasa.Jambo moja kati ya hayo ni tabia halisi ya wajerumani:Hii ni tabia kama desturi ilivyo huchomoza mara moja mtu na kutupa turufu mezani inayolinganisha hali ya sasa na ya wakati wa utawala wa kinazi.Kuhusu azma ya Bw.Wolffsohn katika kufanya hivyo, mtu aweza tu kuvumisha makusudio yake:Kwavile tayari siku za nyuma mara nyingi akigonga vichwa vya habari kwa ulimi wake mwepesi, yafaa kudhania akitaka tu umaarufu.
Kuhusu ziara ya Kanzela Gerhard Schröder nchini Uturuki,gazeti la NORDBAYERRISCHE KURIER linalochapishwa mjini Bayreuth lageukia upande wa kiuchumi wa ziara hiyo.
Laandika:
„Bila ya shaka ,Uturuki inaelewa kwamba kustawi haraka kwa uchumi wake, kutanawirisha juhudi zake za kutaka uwanachama wa Umoja wa Ulaya.Ikiwa inataka kuwafurahisha watiaji-raslimali nchini mwake, basi haitaweza kuepuka kuregeza kamba katika jamii na kutoa uhuru mkubnwa zaidi.
Kanzela Schröder alimbainishia waziri mkuu wa uturuki Erdogan ukweli huu kinaganaga.Amefanya hivyo, kwavile, Schröder anaamini kujiunga kwa Uturuki na UU kutaleta manufaa makubwa kwa Umoja huo.“
Kuhusu azma ya Uturuki kuwa mwanachama wa UU, gazeti la MÄRKISCHE ORDERZEITUNG kutoka Frankfurt Order laandika:
„Kwa kuinadharisha Uturuki ibadili mawazo yake ya kizamani ,Kanzela Schröder ,ameungama ingawa sio moja kwa moja, nchi hii haifai kuwa mwanachama wa UU na kwamba mambo ni magumu zaidi kuweza kuamuliwa na azimio la chama tu . Hatahivyo, haitoshi,kwa serikali ya Ujerumani inayojikuta katika hali ya shinikizo hivi sasa na kuchoshwa na kupanuka zaidi kwa Umoja wa Ulaya ,anapunguza kasi hoja zake.Mbali na hoja za utulivu wa kijiografia kutoka pale Uturuki ilipo karibu na Ulaya –kwa nchi ya kiislamu-hoja ambayo ingeihusu hata Morocco, hakuna sababu halisi ya kuipa Uturuki uwanachama wa Umoja wa Ulaya-laandika gazeti.
Likitumalizia, gazeti la STUTTGARTER NACHRICHTEN laandika:
„kuna mambo mengi yanayotoa hoja zaidi na zaidi kwamba mustakbala wa Uturuki barani ulaya utakua na manufaa kwa pande zote mbili ikiwa utawekwa chini ya msingi wa ushirika wenye nafuu maalumu.Nas hoja hii ni sawa hata ikiwa,kanzela Schröder ,wiki 3 kabla ya uchaguzi katika mkoa huu wa Northrhein-Westfalia ambako kuna kura (180.000 za waturuki) hangebadili maoni yake na kukubali hivyo….