Mjadala wa kupiga marufu AfD unakumbushia enzi za Kinazi
5 Julai 2025Matangazo
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kikundi cha wabunge wa chama hicho mjini Berlin, Weidel amesema hatua hiyo inakumbusha nyakati za kupiga marufuku vyama vingine, chini ya utawala wa Kinazi na kubana uhuru wa vyombo vya habari.
Chama cha SPD kilipitisha azimio katika mkutano wake wa chama wiki iliyopita, kikisema ni wakati wa vyombo vya kikatiba vyenye mamlaka ya kuwasilisha maombi kuanza mchakato wa kutangaza kutokubaliana kikatiba na chama cha AfD.
Marufuku ya chama inaweza tu kuamuliwa na Mahakama ya Katiba ya Shirikisho baada ya ombi rasmi kuwasilishwa na serikali ya shirikisho au mojawapo ya mabaraza ya mabunge.