Utawapata vijana katika mitandao ya kijamii lakini kwenye majukwaa halisi ya kisiasa utawapata kwa kiwango si cha kuridhisha, hili linawafanya wanasiasa kutumia majukwaa ya mitandao kueneza ujumbe wa kisiasa. Lakini je hilo linaweza kubadili mtazamo wako wa kisiasa?