Misri na Sudan: Bwawa la Ethiopia ni kitisho kwa uthabiti
4 Septemba 2025Matangazo
Misri an Sudan zimekubaliana kwamba bwawa la Ethiopia linakiuka sheria ya kimataifa, lina athari mbaya sana kwa nchi hizo mbili upande wa chini na linasimamia kitisho endelevu kwa uthabiti wa hali katika bonde la mashariki la mto Nile kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa kufuatia mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje na wa umwagiliaji wa Misri na Sudan mjini Cairo jana Jumatano, nchi hizo zilisema hatari zilizopo zinatokana na hatua za Ethiopia kulijaza na kuliendesha bwawa hilo, wasiwasi kuhusu usalama wa bwawa na vitisho vya maji kuachiliwa bila udhibiti na kusimamia vyema nyakati za ukame.
Misri na Sudan zimesema Ethiopia lazima ibadili sera yake kurejesha ushirikiano kati ya nchi hizo tatu.