Misaada ya nchi za kigeni yaanza kuwasili Iran
27 Desemba 2003Matangazo
BAM: Makundi ya Kiiran ya kuokoa maisha katika jimbo la Kerman lililoshambuliwa na mtetemeko mkubwa wa ardhi, hivi sasa wameanza kupata misaada ya kwanza kutoka nchi za nje. Makundi mbali mbali ya wasaidizi yamewasili Iran kutoka orodha ya nchi za nje ili kuchangia katika kazi za kutafuta na kuokoa watu pamoja na kusambaza misaada hasa katika mji wa Bam, ulioteketezwa karibu wote. Nao wasaidizi wa Kijerumani kutoka Shirika la Misaada ya Kiufundi la Kijerumani na Shirika la Huduma la Maltese, wamekwisha jiunga na kazi za usaidizi katika eneo la maafa. Mbali na nchi za UU na UM, misaada imeahidiwa pia na Marekani, Urusi, Uchina na Japan. UM umearifu kuweko mahitaji makubwa ya madawa, mablangeti, mahema na magari yenye mazahanati, mitambo ya kutengenezea maji ya kunywa pamoja na majenereta ya umeme.