Misaada ya nchi tat u kwa Iraq:
7 Februari 2004Matangazo
BERLIN: Ujerumani, Ufaransa na Japan zinadhamiria kusaidia ukarabati wa Iraq kufuatana na mpango mkubwa wa miradi ya ushirikiano. Serikali za nchi hizo tatu zimeshauriano juu ya mpango huo wa uishirikiano pamoja na Iraq. Mjini Berli ilithibitishwa ripoti ya jarida la DER SPIEGEL kuhusu mpango huo wa ushirikiano. Naye Kansela Gerhard Schröder anauzungumza mpango huo pamoja na Rais George W. Bush wakati atakapoizuru Marekani mwishoni mwa mwezi huu. Jarida hilo liliendelea kuandika, kufuatana na mpango huo, imewafikiwa kuwa mpaka mwishoni mwa mwaka 2005, Ujerumani itatoa mafunzo kwa polisi 2,000 wa Kiiraq katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Pia Ujerumani itachangia katika uundaji wa shule mpya za mafunzo ya kazi. Lakini mbele kabisa mpango huo wa Ujerumani, Ufaransa na Japan utaendeleza usambazaji wa maji na nishati nchini Iraq.