Miripuko mkutano wa M23 Bukavu yauwa 11
28 Februari 2025Mripuko wa kwanza ulizuwa taharuki kubwa na kusababisha watu kukimbia ovyo ovyo, kabla ya mripuko mwengine kutokea, huku shirika la habari la AFP likiripoti kushuhudia vidimbwi vya damu katika mji huo wa Bukavu.
Rais Felix Tshisekedi ameiita miripuko hiyo kuwa ni tendo la kikatili la kigaidi katika eneo hilo la mashariki mwa nchi yake, ambako waasi wa M23 wametwaa maeneo makubwa ya ardhi katika wiki za hivi karibuni.
Soma zaidi: Karim Khan: Mfumo wa haki wa Kimataifa umeshindwa kukomesha ukatili Kongo
Msemaji wa kundi hilo, Willy Ngoma, alisema viongozi wenzake ndio waliolengwa na mashambulizi hayo, ingawa wote walinusurika.
Mkutano huo ulikuwa umehudhuriwa na kiongozi wa muungano wa makundi ya waasi, Corneille Nangaa.
Hadi sasa, hakuna kundi upande uliodai kuhusika wala sababu ya miripuko hiyo haijajulikana.