Miripuko mikali yasikika kusini magharibi mwa Iran
21 Juni 2025Matangazo
Ahvaz ni mji mkuu wa mkoa wa Khuzestan, ambao uko kwenye mpaka wa Iraq na ndilo eneo kuu la uzalishaji wa mafuta la Iran. Awali jeshi la Israel lilitangaza kuishambulia miundombinu ya kijeshi katika eneo hilo la kusini magharibi.
Wakati huo huo, wizara ya afya ya Iran imesema mashambulizi ya Israelnchini humo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400 tangu kuzuka kwa mapigano wiki iliyopita kati ya mataifa hayo mawili hasimu.
Maelfu ya Wairan waandamana kuipinga Israel
Kwenye chapisho katika mtandao wa X, msemaji wa wizara hiyo Hossein Kermanpour, amesema kufikia leo asubuhi, mashambulizi hayo yamesabababisha kuwepo kwa majeruhi 3,056 ambao wengi wao wamejeruhiwa kwa makombora na droni.