MIRANSHAH: Wanamgambo wauawa nchini Pakistan
13 Machi 2005Matangazo
Vikosi vya usalama nchini Pakistan hii leo vimeshambulia kundi linalodhaniwa kuwa ni la wapiganaji wa kigeni wa al-Qaeda.Opresheni hiyo ilianzishwa baada ya ripoti za upelelezi kuonya kuwa idadi fulani ya watu wanaoshukiwa kuwa na mafungamano na al-Qaeda wanajificha milimani katika kijiji cha Mana katika jimbo la Kaskazini la Waziristan,kiasi ya kilomita 300 kusini-magharibi mwa mji mkuu Islamabad.Wiki iliyopita katika eneo hilo,wanajeshi wa Pakistan waliwauwa washukiwa wawili wa al-Qaeda waliokuwa raia wa kigeni.