Mikusanyiko ya mazishi marufuku DRC
2 Aprili 2020Hatua ya kupiga marufuku mikusanyiko ya watu katika juhudi za kupambana na ugonjwa wa COVID-19 imeathiri utamaduni wa mazishi kwenye baadhi ya makabila ya Congo. Lakini raia wengi wanaomba hatua hiyo iendelee kutekelezwa hata baada ya kumalizika kwa ugonjwa wa Corona kutokana na kwamba utamaduni huo wa kukesha na maiti kabla ya kuzikwa iligeuka kuwa ni biashara na sherehe zilizogarimu fedha nyingi hata kwa familia maskini kabisa.
"Nilifiwa na ndugu yangu." Msemo huo ulikuwa ukitumiwa sana mjini Kinshasa kabla ya kuripuka kwa Corona, kuliko hata misemo mingine mfano wa "Nilialikwa kwenye harusi," "Naenda kanisani," au "Naenda kukutana na rafiki kwenye mkahawa."
Jiji la Kinshasa lenye zaidi ya wakaazi milioni kumi, taarifa za vifo mara nyingi hutangazwa kupitia televisheni na redio. Utamaduni kwenye maeneo ya magharibi mwa Congo ni kwamba anapofariki mtu, msiba hufanyika katika maeneo ya umma ambayo yanakodishwa na familia ya marehemu.Gharama kubwa zinatumika kuanzia kutengeneza vitenge na T-Shirts zenye sura ya marehemu.Kukiwa na waalikwa ambao pia wamevaa mavazi maalumu ya msiba.
Familia zingine huzuwiya barabara hadi sherehe ya mazishi itakapo malizika.
"Ni mahala pa kukutana na wengine huanzisha uhusiano wa kimapenzi ,panakuzwa pia nihapo uhusiano wa jamii. Ni mahala pa majadiliano," alisema Leon Tshambu mtaalamu wa maswala ya jamii nchini Congo.
Sherehe za watu wengi pia marufuku
Tarehe 18 machi, rais Felix Tshisekedi alipiga marufuku maandalizi ya mazishi kwenye maeneo ya umma au majumbani . Alisema maiti yatapelekwa moja kwa moja kutoka chumba cha kuhifadhia maiti hadi makaburini, huku maiti hao wakisindikizwa na watu wachache tu.
Ili kuepuka kusambaa kwa kirusi cha corona, rais Tshisekedi alipiga marufuku mikusanyiko ya watu wengi, na hata sherehe ya zaidi ya watu 20. Shule, makanisa ,mikahawa na vilabu vya kuuza pombe vilifungwa.
Hatua hiyo ya kupiga marufuku mazishi ya hadhara imewasikitisha baadhi ya raia wa Congo.
Francois Okondamomba anayefanya kazi kwenye televisheni ya taifa mjini Kisangani, kaskazini mwa mashariki mwa Congo amesema kwamba watu wameghadhibishwa na hatua hiyo ya kupiga marufuku mizishi ya watu wengi.
Mjini Goma, Kivu ya Kaskazini, pia, Jean Bosco Kaponirwe aliefiwa ndugu yake amesema kwamba haelewi vipi kuwafasiria ndugu zake wengine kwamba hawatohuzuria mazishi hayo kwa sababu ya kuepuka ugonjwa wa Corona.
Mabonga Bonga,chifu wa jadi wa kabila kongwe nchini Congo la wa Pende, mjini Kikwit kusini magharibi mwa nchi mehoji pia hatua hiyo ya serikali na kusema ikiwa ni chifu wa jadi anayefariki mnamo kipindi hiki, je utamaduni wa mazishi ya chifu utatekelezwa au hapana?
Mazishi ya wathirika wa Ebola huko Beni, jimboni Kivu ya kaskazini mara ningi yalisabaisha tofauti baina ya wafamilia na wafanya kazi wa shirika la msalaba mwekundu wanaohusika na mazishi ya wathirika hao.
Congo tayari imerikodi vifo 11 kutokana na ugonjwa wa Corona kiwemo mshauri wa rais Tshisekedi na kiongozi wa zamani wa mawakili wa Congo ambao walitakiwa kuzikwa kwa heshma, lakini mazishi yao yalifanyika siku hiyo hiyo.