JamiiAsia
Miili zaidi yatafutwa katika eneo la ajali ya ndege India
13 Juni 2025Matangazo
Watu zaidi ya 240 waliuawa kwenye ajali iliyohusisha ndege aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la India.
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kwamba India inafikiria kusitisha matumizi ya ndege hizo kwa ajili ya kuzifanyia ukaguzi wa usalama wa ndege hizo.
Ajali ya ndege yaua zaidi ya watu 200 India
Waziri mkuu wa India Narendra Modi alitembelea hii leo katika jimbo la Gujarat, eneo ilikotokea ajali hiyo ambako ni nyumbani kwa waziri mkuu huyo.
Mtu pekee aliyenusurika kati ya watu242 waliokuwemo ndani ya ndege ya abiria iliyokuwa ikielekea London amesema hata yeye anashangaa jinsi alivyonusurika kimuujiza katika ajali hiyo ya ndege.