JamiiAsia
Waliokufa kwenye ajali ya ndege kukabidhiwa familia
16 Juni 2025Matangazo
Maafisa wa afya nchini India wameanza utaratibu wa kuikabidhisha kwa familia zao miili ya watu waliokufa kwenye ajali ya ndege ya shirika la ndege la India wiki iliyopita.Miili zaidi yatafutwa katika eneo la ajali ya ndege India
Hata hivyo, imeelezwa kwamba kufikia leo Jumatatu, familia nyingi za waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo, bado zinasubiri majibu ya uchunguzi wa vinasaba ili kuwatambua wapendwa wao.
Baadhi ya waliofiwa tayari wameshafanya maziko. Watu 279 waliuawa na abiria mmoja alinusurika baada ya ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mjiniLondon, Uingereza, kuanguka na kuwaka moto kwenye eneo la makaazi ya watu muda mfupi baada ya kuruka, watu 38 waliokuwa kwenye eneo hilo pia waliuawa.