Miili yagunduliwa karibu na walipokufa mamia kwa kufunga
22 Agosti 2025Matangazo
Kamishena wa kaunti ya kilifi Josephat Biwott ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa miili ya watu hao watano imepatikana katika makaburi 4 akiongeza kuwa wamepata miili zaidi katika maeneo mengine 27.
Shughuli ya ufukuaji bado inaendelea katika eneo hilo lililoko viungani mwa mji wa Malindi, karibu na eneo la Shakahola ambako mamia ya waumini waliokuwa wanashurutishwa kufunga, walipatikana wakiwa wamefariki, miaka miwili iliyopita.
Mnamo mwezi Julai, afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ya Kenya ilisema inaamini wahanga waliozikwa katika eneo hilo, walilazimishwa kufunga kutokana na kushiriki na kuamini itikadi kali za kidini. Washukiwa 11 wanachunguzwa kuhusiana na vifo hivyo.